Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana ameshinda katika uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Jumatano wiki hii.
Rais Masisi kutoka Chama cha Botswana Democratic Party (BDP) ameshinda kiti cha Urais baada ya kupata asilimia 51 ya kura zote zilizopigwa.
Chama cha BDP ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka 1966, pia kimeshinda viti 29 vya Ubunge.
Rais Masisi ambaye ataiongoza Botswana kwa kipindi kingine cha miaka Mitano, ameahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo hasa rushwa na urasimu kwa Wafanyabiashara.
Zaidi ya Raia Milioni Mbili wa Botswana walijiandikisha kwa ajili kupiga kura katika uchaguzi huo wa Rais, Wabunge na Viongozi wa Serikali za Mitaa.
