Watu 27 wameuawa na wengine zaidi ya hamsini wamejeruhiwa baada ya kutokea kwa mlipuko katika uwanja wa ndege uliopo kwenye mji wa Aden nchini Yemen.
Mlipuko huo umetokea muda mfupi baada ya ndege moja kutua katika uwanja huo, ikitokea nchi jirani ya Saudi Arabia.
Habari kutoka Yemen zinaeleza kuwa, Wafanyakazi wa kutoa msaada na maafisa wa uwanja huo wa ndege, ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa.
Maafisa wa Serikali ya Yemen wamehusisha mlipuko huo na ugaidi, na kuwashutumu Waasi wa Houthi kwa kuhusika na tukio hilo.