Mlipuko katika bomba la mafuta wasababisha vifo Misri

0
776

Watu Saba wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya kutokea mlipuko mkubwa katika bomba la mafuta nchini Misri.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa, kabla ya kutokea kwa mlipuko huo, watu hao walionekana wakichota mafuta kutoka kwenye bomba hilo la mafuta lililokuwa likivuja.

Habari zaidi kutoka nchini Misri zinaeleza kuwa, vikosi vya uokoaji na zimamoto vya nchi hiyo vilitumia takribani saa Tatu kuzima
moto huo uliotokea baada ya mlipuko huo.