Takribani watu 17 wameuwawa baada ya mlipuko mkubwa kutokea karibu na mji maarufu kwa uchimbaji madini huko Ghana magharibi.
Polisi wamesema gari lililokuwa limebeba milipuko kwa ajili ya uchimbaji madini liligongana na pikipiki karibu na mji wa Bogoso.
Picha zilizoonyeshwa na kituo cha habari cha eneo hilo zimeonyesha moshi mkubwa mweusi ukitoka katika majengo yaliyoungua huku mabaki ya majengo hayo yakiwa yametapakaa
Video zinazotisha zinaonyesha miili ya waliofariki ilivyoharibika vibaya.
Pia shimo kubwa lililotokana na mlipuko huo linaonekana kando mwa barabara.
Rais was Ghana Nana Akufo-Addo amesema jeshi limeingia kuongeza nguvu ili kudhibiti madhara zaidi huku kikosi cha dharura nchini humo nacho kimepewa Kazi ya kuongeza msaada wa haraka kwa wakazi wa eneo hilo.