Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha mkutano wa dharura kujadili hatua ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kombora la kisasa la masafa marefu, hatua ambayo imeelezwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa za majaribio ya silaha.
Nchi zinazapakana na Korea Kaskazini zimekutana kwa dharura baada ya nchi hiyo kufanya jaribio lake la kombora la masafa marefu ambalo linaonekana kuwa na mafanikio makubwa.
Hilo ni kombora la kwanza lenye mafanikio makubwa baada ya kombora lingine kama hilo lililofanyiwa majaribio miaka minne iliyopita.
Kombora la hivi karibuni lina uwezo wa kwenda hadi nchini Marekani, hali ambayo imeanza kuleta wasiwasi katika nchi majirani.
Korea Kaskazini mara kadhaa imekuwa na mazungumzo na Korea Kusini pamoja na Marekani kuhusu mpango wake wa makombora ya nyuklia na kuahidi kuwa itapunguza uzalishaji na majaribio ya silaha hizo.