Mkutano wa G20

0
493

Mkutano wa viongozi kutoka mataifa tajiri Duniani maarifu G20,unafanyika huko Osaka nchini Japan ambapo vita ya kibiashara kati ya Marekani na China vinataraji kujadiliwa kwa kina katika mkutano huo.


Mkutano huo ambao hujumuisha Umoja wa Ulaya kama mwanachama, pia utajadili suala la mabadiliko ya Tabia Nchi na umuhimu wa nchi wanachama wa G20 katika utekelezaji wa makubaliano mbalimbali kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.


Suala la mgogoro wa Marekani na Iran unaohatarisha kuzuka kwa mapigano pia linatarajiwa kujadiliwa kwa kina katika mkutano huo wa siku mbili wa Mataifa ya G20 huko Osaka Japan.