Mke wa Rais wa Namibia atangaza kugawa utajiri wake akifariki

0
548

Katika kuondoa mifumo ya ubaguzi na kukosekana usawa kati ya wanaume na wanawake nchini humo, mke wa Rais wa Namibia aamua kuchangia mali zake zote kwa watu wenye uhitaji pindi atakapofariki.

Monica Geingos anatarajia kugawa utajiri wake unaokadiriwa kuwa na thamani ya Tsh 6.9 bilioni akiwa na lengo la kubadili namna ambazo wake wa marais hukabiliana na ubaguzi katika nchi zao.

Pindi atakapofariki utajiri wake wote utahamishiwa kwa taasisi yake ya One Economy Foundation, ambayo ndiyo itahusika na ugawaji wa fedha hizo kwa watu mbalimbali wenye uhitaji.

Taasisi hiyo hukopesha fedha kwa wajasiriamali, hutoa mikopo kwa wanafunzi na kuwasaidia wahanga wa matukio ya unyanyasaji wa kijinisa, ambapo wajumbe wa bodi ya taasisi hiyo ni pamoja na walinzi na wafanyakazi wa majumbani.

Monica amekanusha madai ya kutaka kutwaa nafasi kubwa ya kisiasa nchini humo kwa maelezo kuwa huhitaji kuwa mwanasiasa kuweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii.