Mji wa Gharyan uliopo Libya wakombolewa

0
504

Vikosi vya jeshi la serikali ya Libya vinavyotambuliwa na Umoja wa Mataifa, vimefanikiwa kuukomboa mji wa Gharyan uliokuwa ukishikiliwa na wapiganaji wa jenerali muasi nchini humo Halifa Haftar.


Taarifa kutoka nchini humo zinaarifu kuwa vikosi vya serikali ya Libya vimeukomboa mji huo uliopo umbali wa kilomita themanini kusini mwa mji mkuu wa Tripol, baada ya mapambano makali kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa jenerali Haftar.


Akizingumzia kukombolewa kwa mji huo wa Gharyan ulikokuwa kituo kikuu cha wapiganaji wa Haftar,Kamanda wa vikosi vya Serikali ya libya Jenerali Mustafa Al Tayib amesema hiyo ni hatua nzuri kwa jeshi la serikali katika kuwadhibiti waasi hao, na kusema kuwa mji huo kamwe hautarejea katika himaya ya Jenerali Halifa Haftar na wapiganaji wake.