Mshindi wa Mashindano ya Miss USA mwaka 2019 Cheslie Kryst amefariki dunia kwa kujiua Jumapili asubuhi akiwa na miaka 30.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na tovuti ya habari za burudani ya TMZ polisi walifika eneo la tukio saa 1:13 asubuhi.Cheslie alitangazwa kupoteza maisha mara tu vikosi vya polisi na madaktari kufika eneo hilo.
Polisi wanachunguza mazingira yaliyopelekea kifo chake, ambapo mpaka sasa inaaminiwa kwamba alijiua, kutokana na maofisa was polisi kuamini kwamba alijirusha kutoka ghorofa la 29.
Saa chache kabla ya kujiua, Cheslie Cheslie aliposti picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa na maelezo “Siku hii ikuletee pumziko na amani”.Polisi wamesema kwamba Cheslie aliacha ujumbe kwamba anaacha mali zake zote kwa mama yake.