Misri yatakiwa kusimamia haki za binadamu

0
1160

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amemtaka Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri kusimamia haki za binadamu nchini humo.

Macron ametoa kauli hiyo mjini Cairo nchini Misri ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini humo, ziara yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya Ufaransa na Misri.

Rais huyo wa Ufaransa amesema kuwa amelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Misri.

Akiwa nchini Misri pamoja na mambo mengine, Macron  ameshuhudia utiwaji saini mikataba 30 ikiwemo ile inayohusu sekta za usafirishaji, elimu na afya baina ya nchi hizo mbili.