Misaada yawasili Venezuela

0
1061

Malori yaliyobeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya raia wa Venezuela, yamewasili kwenye mpaka wa nchi hiyo na Colombia.

Misaada hiyo imewasili wakati  huu ambapo nchi kadhaa za Ulaya na zile za Amerika ya Kusini zikimtaka Rais Nicolas Maduro wa Venezuela kuitisha uchaguzi huru wa urais.

Habari kutoka nchini Venezuela zinasema kuwa malori kadhaa yaliyobeba chakula na dawa kutoka nchini Marekani yamewasili kwenye  eneo la  Tienditas ambalo ni la mpaka kati ya Venezuela na Colombia.

Wakati hayo yakiendelea, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Migogoro (ICG) limesema  kuwa liko tayari kutafuta amani nchini Venezuela kwa njia za Kidiplomasia.

Venezuela imeingia kwenye mgogoro wa kisiasa wa kugombania madaraka baina ya Rais  Nicolas Maduro na Kiongozi wa upinzani nchini humo  Juan Guaido ambaye pia amejitangaza kuwa Rais wa mpito.