Milipuko Sri Lanka yaua watu 137

0
388

Watu 137 wameuawa na mamia wengine wamejeruhiwa katika mfululizo wa mashambulio dhidi ya makanisa na hoteli nchini Sri Lanka.

Habari kutoka nchini Sri Lanka zinasema kuwa milipuko Sita imeripotiwa katika makanisa Matatu yaliyopo kwenye miji ya Kochchikade, Negombo na Batticaloa wakati wa Ibada ya Pasaka.

Hoteli za The Shangri La, Cinnamon Grand na Kingsbury ambazo zipo mjini Colombo, pia zililengwa katika mashambulio hayo.

Hadi sasa hakuna mtu wala kundi lolote lililolodai kuhuhusika na mashambulio hayo.