Miili ya marehemu kugeuzwa kuwa mboji (mbolea)

0
398

New York imeidhinisha utengenezaji wa mboji itokanayo na miili ya binadamu.

Utengenezaji wa mboji kwa kutumia miili ya binadamu unaonekana kuwa mbadala wa mazingira rafiki wa mazishi au kuchoma maiti.

Hivi sasa New York imekuwa jimbo la kwanza kwa Marekani kuruhusu kuugeuza miili ya binadamu kuwa udogo baada ya kifo chake kwa njia inayojulikana kama “upunguzaji wa kikaboni asilia,” ambapo mwili utaoza baada ya kufungwa kwenye kontena.

Utengenezaji huo wa mboji utagharimu muda wa mwezi mmoja baada ya mchakato wa kuuwa vimelea vya maambukizi ya magonjwa yoyote na ndugu za mrehemu watapatiwa udongo huo ambao wanaweza kuutumia kuoteshea maua, mbogamboja na miti.