Mfahamu mwanamke mweusi wa kwanza kuwa mhariri wa magazeti

0
260

Miaka 197 iliyopita Oktoba 9, 1823 alizaliwa  Mary Ann Shadd Cary mwenye asili ya Marekani na Canada.

Cary ni mwanamke mweusi wa kwanza Amerika Kaskazini na mwanamke wa kwanza nchini Canada kuwa mhariri wa magazeti.

Jambo hili ukizingatia hali ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendelea kipindi hicho hasa Marekani ambayo imesheheni watu weupe, Cary alikuwa na ujasiri wa kipekee kupigania hadi kufikia ngazi hiyo ya uhariri.

Kabla ya kuwa mwanamke wa rangi wa kwanza kuwa mhariri Amerika Kaskazini, Cary alikuwa ni mwalimu na baadaye akachukua shahada ya sheria na kuwa mwanamke wa pili mwenye shahada ya sheria nchini Marekani.

Mwaka 1853 Mary Ann Shadd Cary aliazisha gazeti lililochapisha habari kuhusu watumwa waliotoroka lililojulikana kwa jina la ‘The Provincial Freeman’ (Mtu Huru wa Mkoa).

Mwaka 1994 Serikali ya Canada ilimtambua Cary kuwa mtu mwenye umuhimu katika historia ya nchi kutokana na mchango wake kwenye jamii na nchi yake.

Cary alifariki dunia Juni 5, 1864 kutokana na saratani ya tumbo.