Mazishi ya kitaifa ya Mwai Kibaki kufanyika leo

0
1032

Mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa tatu wa Kenya, Mwai Kibaki yanafanyika leo katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Watu mbalimbali mashuhuri, Viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Kenya, Mabalozi na Wananchi wa kawaida wanashiriki katika mazishi hayo.

Katika mazishi hayo ya kitaifa ya Rais mstaafu Mwai Kibaki, Rais Samia Suluhu Hassan anawakilishwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ambaye tayari ameondoka nchini kuelekea jijini Nairobi.

Kabla ya kufanyika kwa mazishi ya Kitaifa katika uwanja wa Nyayo, mwili wa Mwai Kibaki umepelekwa kwenye Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi, ikiwa ni heshima kwa kiongozi huyo kwa kuwa aliwahi kuwa Rais wa Taifa hilo.

Mazishi rasmi ya Mwai Kibaki aliyefariki dunia tarehe 21 mwezi huu akiwa na umri wa miaka 90, yanafanyika hapo kesho huko Nyeri.