Mawaziri wahukumiwa kwenda Jela

0
445

Mahakama nchini Algeria imewahukumu kwenda jela mawaziri wawili wa zamani wa nchi hiyo pamoja na aliyekuwa spika wa bunge la nchi hiyo kwa makosa ya rushwa .

Hukumu hiyo inakuja ikiwa siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika alkhamis baada ya nchi hyo kuongozwa na serikali ya mpito tangu alipoondoka madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abdelaziz Boutteflika kwa kushinikizwa na wananchi.

mahakama hiyo imemhukumu aliyekuwa Waziri Mkuu  Ahmed Ouyahia kwenda jela miaka 15  , Abdelmalek Sellal miaka 16 pamoja na faini ya dola elfu 24   huku aliyekuwa spika wa bunge Moad Bouchareb  kutumikia kifungo cha miaka ishirini jela.

Mawaziri hao wanatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao na uhujumu uchumi lakini wamekanusha kuhusika na kashfa hizo.

Habari zinaeleza kuwa hii ni mara ya kwanza tangu nchi hiyo ipate uhuru  mawaziri wakuu kuhukumiwa kwenda jela.