Matokeo ya Urais Kenya kutangazwa muda wowote

0
176

Siku saba za kikatiba ilizopewa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC) kutangaza mshindi wa kura za urais zinamalizika hapo kesho.

Wakati saa chache zikiwa zimesalia kumalizika kwa muda huo, mwonekano wa ukumbi wa Bomas unaotumika kuhakiki na kutangaza matokeo umekuwa na mwonekano tofauti, na inatarajiwa muda wowote kuanzia sasa mshindi anaweza kutangazwa.

Katika kinyang’anyiro hicho cha Urais, upinzani mkubwa umekuwa kati ya Raila Odinga kutoka muungano wa Azimio la Umoja na William Ruto kutoka muungano wa Kenya Kwanza ambaye pia ni Naibu Rais wa Kenya katika serikali inayomaliza muda wake.