Mataifa mbalimbali kujadili moto katika misitu ya Amazon

0
298

Mataifa mbalimbali yaliyopo Amerika ya Kusini yanatarajiwa kukutana Tarehe Sita mwezi Septemba mwaka huu, kwa lengo la kujadili tatizo la moto unaoendelea kuwaka katika misitu ya Amazon iliyopo nchini Brazil, misitu ambayo imekua ikitegemewa kwa kiasi kikubwa na Mataifa hayo.

Mkutano huo unafanyika katika kipindi ambacho Rais Jair Bolsonaro wa Brazil,amekubali kupokea msaada wa Kimataifa kwa ajili ya kuuzima moto huo, msaada ambao awali aliukataa.            

Rais Bolsonaro amewaambia Waandishi wa habari kuwa, mkutano huo ambao utajadili sera mbalimbali zitakazosaidia kuilinda misitu hiyo ya Amazon, utafanyika katika mji wa Leticia nchini Colombia.

Mataifa yatakayoshiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na Argentina, Peru,Colombia, Chile, Bolivia, Ecuador na Uruguay.

Hata hivyo Rais huyo wa Brazil, – Jair Bolsonaro amesema kuwa Venezuelahaitashiriki katika mkutano huo wenye lengo la kujadili tatizo la moto unaoendelea kuwaka katika misitu ya Amazon iliyopo nchini Brazil