Hali ya wasiwasi imeongezeka nchini Uingereza, baada ya matukio ya mashambulio ya visu yanayosababisha mauaji kuongezeka.
Habari kutoka nchini Uingereza zinasema kuwa, tangu kumalizika kwa vita kuu ya dunia ya pili nchini humo, matukio ya watu kushambuliwa kwa visu na kuuawa yamekuwa yakiongezeka kila siku.
Katika kipindi cha hivi karibuni, watu Mia Saba wamekufa kwa kushambuliwa na visu nchini humo.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, tayari watu Thelathini wamekufa nchini Uingereza katika matukio ya kushambuliwa na watu wenye visu na kila baada ya siku moja na nusu, kuna mtu anakufa baada ya kushambuliwa kwa kisu au visu.
Utafiti unaonyesha kuwa, mara nyingi vijana ndio wanajihusisha na matukio ya kushambulia watu kwa visu na kuwaua.
