Serikali ya Marekani imethibitisha kuwa watu sita na watu wengine wawili waliohusika na mauaji katika mji wa New Jersey, nchini humo wameuawa baada ya kutokea mashambulio ya bunduki katika mji huo.
Habari zinasema watu wenye silaha walifanya mashambulio ya makusudi katika mji huo na kuwaua watu sita huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. Polisi walifanikiwa kuwapiga risasi na kuwaua watu wawili waliohusika na shambulio hilo la bunduki.
Habari zinasema hali ya utulivu imerejea katika mji huo wa New Jersey na polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Nchi ya Marekani mara kadhaa imeshuhudia mashambulio ya bunduki, yaliyosababisha vifo vya watu na wananchi kutaka serikali ya nchi hiyo kupitisha sheria ya kudhibiti udhibiti wa silaha miongi mwa raia.
