Marekani yawaachia kwa muda wahamiaji mia tatu

0
371

Idara ya uhamiaji nchini Marekani imewaachia kwa muda, takribani wahamiaji mia tatu kati wahamiaji mia saba waliokamatwa kufuatia oparesheni maalumu iliyofanyika siku ya Jumatano wiki hii huko Mississippi.

Wahamiaji hao walioachiwa kwa muda ni wale wenye watoto wadogo waweze kutoa huduma ya malezi kwa watoto wao walioingia nao nchini Marekani kutafuta shughuli za kuendesha maisha yao.

Hatua ya kuachiwa kwa muda kwa wahamiaji hao, inatokana na Wabunge wa Chama Cha DEMOCRAT cha nchini Marekani, kulaani ukamatwaji wa wahamiaji hao ambao baadhi yao walitenganishwa na watoto wao.