Vikosi vya Marekani vimefanya shambulizi dhidi ya wanamgambo wa Al Shabaab na kufanikiwa kuwaua wanamgambo 4 wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Kigaidi la Al Shabaab
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema jeshi lake barani Afrika, US Africa Command na AFRICOM wamefanya Mashambulio yaliyowalenga wanamgambo hao wa Al Shabaab nchini Somalia ambao wanaendelea kuwaua raia.
Shambulio hilo limetekelezwa ikiwa imepita wiki moja baada ya kundi la Al Shabaab kufanya shambulio katika Mji mkuu wa Mogadishu na kuua watu 79 na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
Wakati huo huo Jeshi la Marekani limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za kundi moja la wanamgambo wenye mfungamano na serikali ya Tehran, na kuua wapiganaji kadhaa.