Marekani yaripoti idadi kubwa ya vifo vya corona

0
198

Marekani imeripoti vifo vya watu Elfu Tatu vilivyosababishwa na ugonjwa Corona katika kipindi cha siku moja.

Habari kutoka nchini Marekani zinasema kuwa, idadi hiyo ya vifo ni ya juu zaidi kuwahi kutokea tangu nchi hiyo ilipokumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo wa Corona.

Kufuatia hali hiyo, tayari mamlaka mbalimbali nchini Marekani zimetoa wito wa kuongeza kasi na juhudi za kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo, ambao unaripotiwa kuenea katika miji mbalimbali.