Mwanasayansi wa Iran ambaye ni kati ya wairan walizuiliwa nchini Marekani ameachiwa huru na yuko safarini kurejea nyumbani.
Dkt. Sirous Asgari alishitakiwa na mahakama moja ya nchini Marekani mwaka wa 2016 kwa tuhuma za wizi wa siri za kibiashara wakati alipokuwa katika ziara ya mafunzo kwenye jimbo la Ohio nchini humo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya Nje wa Iran, Abbas Mousavi amesema Dkt. Asgari ambaye ni mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif mjini Tehran alifutiwa mashitaka mwezi Novemba mwaka jana.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Iran ilisema mwezi uliopita Asgari ameambukizwa virusi vya Corona wakati akiwa kizuizini.