Marekani yakiri wanajeshi wake kujeruhiwa Iraq

0
595

Serikali ya Marekani imekiri kuwa wanajeshi wake 11 walijeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na Iran katika kambi ya jeshi la wanaanga ya Ain al-Assad nchini Iraq Januari 8.

Kamanda wa kikosi hicho amesema askari hao wanatibiwa na wengine kufanyiwa uchunguzi.

Awali Rais Donald Trump alisema hakuna mwanajeshi yeyote wa marekani aliyejeruhiwa kutokana na shambulio hilo.

Wiki chache zilizopita Iran ilirusha makombora katika kambi za Ain al-Assad na Erbil nchini Iraq baada ya kifo cha Jenerali wa jeshi la Iran Qassem Soleimani, ambapo baadhi ya wanajeshi 5,200 wa Marekani walikuwa katika kambi hizo.