Marekani na Korea Kaskazini waendelea kuvutana kuhusu nyuklia

0
450

Mwakilishi wa Marekani katika mazungumzo ya nyuklia Stephen Biegun amesema nchi yake haitokubali muda wa mwisho uliowekwa na Korea Kaskazini wa kufikia makubaliano kwenye mazungumzo ya nyuklia yaliyokwama na kuitaka nchi hiyo kerejea haraka katika meza ya mazungumzo.

Amesema ingawa wanatambua kuwa Pyongyang inaweza kuamua lolote katika siku zijazo lakini haitosaidia kutafuta amani ya kudumu kwenye rasi ya Korea.

Biegun ambaye alikuwa mjini Seoul kwa mazungumzo na maafisa wa Korea Kusini ametoa wito kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kufanya mazungumzo tena ili kukamilisha mafanikio yaliyopatikana.

Hadi sasa serikali ya korea kaskazini haijatoa tamko lolote juu ya mazungumzo hayo ya nyukilia.