Mapigano yasababisha njaa

0
376

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema Wananchi katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia wanakabiliwa na njaa, kutokana na mapigano kati ya majeshi ya nchi hiyo na waasi katika jimbo hilo.
 
WFP imesema juhudi za haraka zinahitajika kuwasaidia Wananchi hao wanaokabiliwa na njaa kutokana na athari za mapigano hayo.
 
Wananchi hao wanakabiliwa na njaa kutokana na mashamba na shughuli nyingi za kiuchumi kuharibiwa na mapigano, huku baadhi yao wakilazimika kuyakimbia makazi yao na kwenda kuishi uhamishoni.