Mamia yajitokeza kuuza figo Kenya

0
203

Hospitali ya Taifa ya Kenya imesema kuwa idadi kubwa ya watu wamejitokeza wakiuliza na kujitolea kuuza figo zao, hali inayohusisha na kupanda kwa gharama za maisha.

Katika chapisho lake la Facebook hospitali hiyo imesema kuwa swali “figo yangu ni shilingi ngapi?” ndilo limeulizwa mara nyingi zaidi kwenye ukurasa wao.

Kutokana na hali hiyo, hospitali hiyo imesema viungo vya binadamu vinaweza kutolewa kwa hiari ili kusaidia wahitaji lakini sio kuuzwa.

“Tafadhali zingatia kuwa uuzaji wa viungo ni kinyume na sheria. Unaweza tu kuchangia kwa hiari,” imeeleza.

Mapema mwezi huu Benki ya Duniani ilitahadharisha kuwa ukanda wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa maeneo yatakayoathirika na vita vya Urusi na Ukraine na janga la UVIKO19.