Mama janeth atunukiwa tuzo

0
359

Mama Janeth Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Kimataifa toleo la tatu, inayotolewa na taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu maarufu M. T. Kasalu, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kwa Taifa la Tanzania na kwa Hayati Rais John Magufuli wakati akiwa madarakani.

Tuzo hizo hutolewa kwa wenza wa viongozi wakuu wa nchi na watu maarufu duniani kwa kutambua michango yao kwa wenza wao, jamii na Taifa husika.