Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Malawi, – Maria Jose Torres amewataka Waumini wa dini mbalimbali nchini humo kujenga tabia ya kuvumiliana ili kuepusha migongano baina yao.
Torres ametoa wito huo kufuatia tukio la kufukuzwa Shule kwa Wanafunzi Wawili wa Kike katika shule ya M’manga iliyopo kwenye mji wa Balaka, kutokana na kuvaa vazi la Hijab, hali iliyosababisha ghasia.
Amesema kuwa, ni muhimu kwa kila Muumini nchini Malawi kuheshimu Uhuru wa kuabudu wa mwenzake na ameshauri yafanyike majadilianao ya Kitaifa ili kushughulikia jambo hilo na kuhakikisha halitokei tena.
Katika vurugu hizo ambazo hasa zilihusisha Waumini wa Dini ya Kiislam na Kikristo, watu kadhaa wamejeruhiwa, huku maduka, misikiti na makanisa yakiharibiwa.