Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaandaa mfumo mzuri wa kulibadilisha shirika la Utangazaji Tanzania ili kuweza kuhimili ushindani wa ndani na nje ya nchi ikiwemo maslahi na miundombinu kwa wafanyakazi
Naibu waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Kundo Adrea Mathew amesema hayo katika mkutano wa siku mbili wa baraza la wafanyakazi wa shirika la Utangazaji TBC kwa mwaka 2021
akiwasilisha mada yake kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi RAAWU Taifa Jane Mihanji amesema baraza la wafanyakazi ni muundo muhimu wa dhana ya ushirikishwa na mahusiano mazuri kazini na vyama pia wafanyakazi ni daraja kati ya wafanyakazi na waajiri
Naye Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayub Rioba Chacha amesema shirika limejipanga kwa maboresho ya miundombinu na mazingira mazuri ya kufanyia kazi kuliko ilivyo sasa
“Tumeendelea na matengenezo ya mitambo maeneo mbalimbali huku tukiendelea kununua vifaa vipya vya kuboresha mawasiliano na utendaji Kazi ili kusikika vizuri ndani na nje ya Nchi” ameongeza Mkurugenzi Mkuu Dkt Ayub Rioba
Baraza la wafanyakazi hupitia maazimio ya baraza lililopita hutazama mipango, bajeti na mawazo ya kuwakilisha wafanyakazi wengine.