Mahakama yahalalisha mlinzi aliyemtaka waziri kupanga foleni kufukuzwa kazi

0
335

Mtumishi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) nchini Kenya ambaye aifukuzwa kazi mwaka 2017 kwa kutomhehsimu aliyekuwa Waziri wa Elimu, Fred Matiang’i, ameangukia pua baada mahakama nchini humo kutupilia mbali kesi yake.

Mahakama imetoa uamuzi huo na kusema kwamba kitendo cha dhihaka alichofanya Daizy Cherogony dhidi ya Dkt Matiang’i kinatosha kwa mwajiri wake, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (KAA), kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake.

Cherogony alifungua kesi dhidi ya KAA kwa madai kuwa kitendo cha yeye kufukuzwa kazi hakikufuata sheria, na pia alidhalilishwa na mwajiri huyo na kutaka alipwe fidia KSh milioni 2.4 (TSh milioni 55).

Amesema katika siku ya tukio, Aprili 5, 2017 abiria uwanjani hapo walikuwa wakipiga kelele, na alipomuona Waziri Matiang’i alimtaka apange foleni kwa ajili ya ukaguzi, na kwamba kitendo hicho hakikukiuka sheria wala taratibu yoyote ya KAA.