Mahakama yaamuru Zuma akamatwe

0
375

Mahakama nchini Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais Mstaafu wa nchi hiyo, Jacob Zuma kutokana na kutofika mahakamani katika kesi ya rushwa inayomkabili.

Rais Zuma alitarajiwa kufika mbele ya Mahakama Kuu ya Pietermaritizburg, lakini hakutokea.

Amedai kwamba asingeweza kufika kwa sababu ni mgonjwa, na kuna taarifa kuwa yupo nchini Cuba kwa ajili ya matibabu, lakini haijaelezwa anasumbuliwa na tatizo gani.

Zuma anatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kampuni ya vifaa vya kijeshi ya Ufaransa, Thales, kupitia kwa mshauri wake wa masuala ya kifedha, Schabir Shaik ambaye alitiwa hatiani kwa makosa ya wizi na rushwa mwaka 2005.