Mafuriko yaua zaidi ya watu 70 Indonesia na Timor Kaskazini

0
185

Zaidi ya watu 70 wamefariki na wengine wengi wahawajulikani walipo baada ya mafuriko na maporomoko ya ardhi kuyakumba baadhi ya maeneo nchini Indonesia na Timor Mashariki.

Msemaji wa Idara ya Kupambana na Majanga ya Indonesia, Raditya Jati amesema kuwa mafuriko hayo yaliyosababisha maafa makubwa yamesababishwa na mvua zinazonyesha nchini humo ambako waokoaji wanaendelea na jitihada ya kusaidia watu walioathiriwa na mafuriko hayo.

Waokoaji wanasema nyumba nyingi, barabara na madaraja vimefunikwa na matope, na kufanya hali kuwa ngumu kwao kujaribu kufikia maeneo yaliyoathiriwa zaidi Mashariki mwa kisiwa cha Flores cha Indonesia.

Maafisa wa uokoaji wanasema huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka kwani hadi sasa watu zaidi ya arobaini hawajulikani walipo. Kwa upande mwingine maelfu ya watu wamekosa makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko.