Watu Kumi wamekufa na wengine kadhaa hawajulikani walipo, baada ya mafuriko makubwa kuikumba nchi ya Misri hasa katika mji wa Alexandria.
Mamia ya watu wamelazimika kubaki katika nyumba zao na kushindwa kwenda kazini, baada ya mitaa mingi ya mji huo kujaa maji na kushindwa kupitika.
Mafuriko hayo pia yameukumba mji mkuu wa Misri, – Cairo.