Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza katika mji wa Bangkok nchini Thailand wakiishinikiza serikali ya nchi hiyo kufanya mabadiliko ya kisiasa.
Watu hao wanataka mabadiliko katika mfumo wote wa kisiasa nchini humo, ukiwemo pia utaratibu wa utawala wa kifalme ambao umedumu kwa miongo kadhaa nchini humo.
Maandamano hayo yanayohamasishwa na wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo yalianza mwezi uliopita.
Waandamanaji wanataka kuwepo kwa marekebisho ya katiba, bunge la nchi hiyo kuvunjwa na kuundwa bunge jipya, ikiwa ni pamoja na marekebisho katika jeshi la nchi hiyo, ambalo mara kadhaa huingilia kati masuala ya kiserikali.