Maelfu wamuaga Mugabe

0
727

Viongozi kadhaa wa Afrika waliohudhuria shughuli ya Kitaifa ya kuuaga Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe,-Robert Mugabe, wamemuelezea Kiongozi huyo kuwa alikua ni Shujaa wa Afrika.


Shughuli hiyo imefanyika katika uwanja wa Taifa wa michezo uliopo Mjini Harare na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Zimbabwe.


Akihutubia Waombolezaji, Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amemuelezea Mzee Mugabe kuwa alikua ni Kiongozi anayeona mbali na kwamba ataendelea kukumbukwa na vizazi vilivyopo na vijavyo nchini humo.


Wakati wa shughuli hiyo ya Kitaifa ya kuuaga Mwili wa Mzee Mugabe , RĂ is Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amelazimika kuomba radhi kutokana na vurugu zilizotokea nchini mwake dhidi ya Wageni, baada ya Waombolezaji kuanza kupiga yowe, hali iliyokua ikisababisha akatishe hotuba hiyo.


Waombolezaji hao walikua wakipiga Yowe ikiwa ni ishara ya kupinga vitendo vya kuwashambulia Wageni. vinavyoendelea nchini Afrika Kusini.