Mamia ya madaktari kutoka nchini Cuba wameendelea kwenda katika mataifa mbalimbali duniani kutoa huduma za kitabibu bure, iki kufanikisha jitihada za kudhibiti kuenea zaidi kwa virusi vya corona.
Serikali ya nchi hiyo leo imeaga timu nyingine ya madaktari tayari kwenda kutoa huduma ya kitabibu katika nchi za Carribean, ambako mapambano dhidi ya virusi hivyo vinavyosababisha homa ya mapafu yanaendelea.
Wiki iliyopita kundi lingine na madaktari lilikwenda nchini Italia kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na corona, ambayo imeendelea kusababisha vifo vya maelfu ya watu.
Madaktari hao wanasema, linapofikia suala la kuokoa maisha ya binadamu, siasa huwekwa kando na kazi kutangulia.
Cuba ndiyo nchi yenye uwiano bora kati ya wagonjwa na madaktari na hivyo kuwa rahisi kutoa huduma hiyo kwa mataifa mengine.