Macron ashindwa uchaguzi wa wabunge

0
132

Chama cha Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kimeshindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge nchini humo.

Muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto ulioongozwa na Jean – Luc Melenchon umeongoza kwa kupata viti vingi bungeni huku chama cha mrengo wa kulia cha National Rally cha Marine Le Pen kikipata viti 89 bungeni.

Kikiwa na viti 245 chama cha Macron kitahitaji kuunda ushirika na vyama vingine ili kiweze kufikisha viti 269 ambavyo vitamuwezesha kuliongoza bunge lenye wabunge 577, hatua ambayo itamuwezesha kiongozi huyo kupitisha sera zake kadhaa na kufanya mabadiliko katika serikali yake.