Mamia ya wananchi wa India wameandamana katika miji mbali mbali nchini humo wakipinga mashambulizi waliyofanyiwa wanafunzi na walimu katika chuo kikuu cha New Delhi.
Waaandamanji hao pia wanapinga ghrama kubwa ya ada za vyuo vikuu nchini humo.
Uvamizi katika chuo kikuu hicho unadaiwa kufanywa na watu wanaolezwa kuvaa mask za uso ambao pia wanahusishwa na chama tawala cha BJP .
Miezi ya hivi karibuni india imekuwa ikikumbwa na maandamano ya mara kwa mara tangu kupitishwa kwa sheria ya uraia inayodaiwa kuwatenga waislamu.