Maelfu ya waandamanaji katika mji wa Hong Kong kwa mara nyingine wamejitokeza katika mitaa mbalimbali ya mji huo, kushiriki katika maandamano ya kupinga hatua ya Polisi kumpiga risasi kijana mmoja aliyeshiriki katika maandamano hayo.
Waandamanaji hao wamekasirishwa na hatua ya Polisi kutumia risasi za moto dhidi ya Waandamanaji, ingawa jeshi la Polisi katika mji huo wa Hong Kong limetetea hatua ya polisi aliyempiga risasi kijana huyo na kusema kuwa ilikuwa ni hatua ya kujihami.
Jeshi la Polisi nchini China limesema kuwa, hali ya maandamano haikuwa shwari na askari huyo kama asingetumia risasi ya moto kujihami, basi yeye ndiye angedhurika.
Waandamanaji hao wamezidi kuonyesha hasira dhidi ya Serikali ya China kwa madai kuwa, Polisi wa kutuliza ghasia wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi kutawanya maandamano yao.