Maambukizi ya corona yaenea kwa kasi Korea Kusini

0
473

Wataalam wa afya Korea Kusini wanaendelea kutafuta njia za kukabiliana na virusi vya corona, ambavyo vimeendelea kuenea kwa kasi nchini humo kwa siku ya pili hii leo.

Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Chung Sye-kyun amesema kuwa hali iliyopo sasa nchini ni humo ni mbaya kwa kuwa zaidi ya watu mia mbili wameripotiwa kuambukizwa virusi hivyo.

Miji ya Daegu na Cheongdo ndiyo imeathirika zaidi, huku maeneo kadhaa ya miji hiyo yakiwa yamewekwa chini ya karantini.

Mapema wiki hii kifo cha mgonjwa wa kwanza wa homa ya corona kimeripotiwa katika mji wa Cheongdo.