Lori laparamia wanafunzi 14 wakivuka barabara

0
294

Wanafunzi wawili wamefariki dunia na wengine 12 wamepata majeraha mbalimbali baada ya lori kuwaparamia mjini Lagos nchini Nigeria.

Taarifa zinaeleza kwamba lori hilo lilipata hitilafu ya breki ndipo dereva akashindwa kuliongoza na hivyo kupoteza mwelekeo.

Mashuhuda wamesema kwamba watoto hao walikuwa wanarejea nyumbani kutoka shule, ndipo wakakumbwa na ajali hiyo wakati wakivuka barabara.

Dereva alijaribu kukimbia baada ya ajali lakini alikamatwa. Vurugu zilitokea eneo hilo ambapo wanafunzi wengine walishambulia magari yaliyokuwa yakipita.

Ajali hiyo imetokea siku tatu tu tangu miili ya watoto nane ilipopatikana ndani ya gari katika sehemu nyingine ya mji huo.