Lebanon waendelea na maandamano

0
844

Kwa mara nyingine, Waandamanaji katika mji wa Beirut nchini Lebanon wamejitokeza katika mitaa mbalimbali ya mji huo kushiriki katika maandamano ya kupinga Serikali na kutaka mabadiliko ya haraka ya kisiasa kufanyika nchini humo.

Licha ya Rais Michel Aoun wa Lebanon kuhutubia Taifa na kusema kuwa atafanya juhudi za makusudi kuhakikisha matakwa ya Waandamanaji, ikiwa ni pamoja mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa yanatakelezwa lakini Waandamaji hao wameendelea na maandamano yao.

Hapo jana Waandamanaji hao walibadilisha mtindo wa maandamano, na kuandamana kwa mtindo wanaouita uzio wa binadamu, kwani walikuwa wakishikana mikono kama ishara ya mshikamano na kudai kuwa wanahitaji mabadiliko kwa ustawi wa maisha yao.