LATRA yakanusha kupanda nauli za mabasi

0
193

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) imekanusha taarifa za ongezeko la nauli kwa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani yanayoanzia safari katika kituo cha mabasi cha Magufuli mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahojiano maalum na TBC, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Gewe amewataka Wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zinazodai kupanda kwa nauli hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Mustafa Mwalongo amesema hakuna nauli iliyoongezeka.