Mji wa Changwon nchini Korea Kusini kuwakopesha wanandoa ili wapate watoto zaidi kutokana na kuwepo kwa upungufu wa watu katika mji huo.
Kiasi cha Won milioni 100 (₩ 100,000,000) takribani shilingi milioni 217 za Kitanzania zitatolewa kwa wawili hao huku riba ikisamehewa kwa wale watakaoamua kupata mtoto mmoja.
Wanandoa wataondolewa 30% ya mkopo huo endapo wataamua kuongeza mtoto wa pili. Lakini pia wanandoa watasamehewa kabisa mkopo huo endapo watapata watoto watatu na zaidi.
Takwimu za ‘populationstat’ zinaonesha mji wa Changwon una watu 1,055,451 kwa mwaka 2021 huku idadi ikionekana kupungua toka mwaka 2005.