Kituo kingine cha kutesa watu chagundulika Nigeria

0
987

Polisi nchini Nigeria wamewaokoa watu 67 waliokua wakishikiliwa na kuteswa katika kituo kimoja kilichopo kwenye mji wa Daura uliopo Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, mji ambao anatoka Rais Muhammadu Buhari.

Habari kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa, watu hao ambao wote ni Wanaume wakiwemo Wavulana wenye umri wa chini ya miaka Saba, wamekutwa wakiwa wamefungwa minyororo,wakiwa na majeraha makubwa baada ya kupigwa na wamethibitisha kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.

Mara baada ya watu hao kuokolewa, kituo hicho kimefungwa na mmiliki wake amekamatwa na Jeshi la polisi nchini Nigeria kwa mahojiano.

Kwa mujibu wa takwimu za nchi hiyo, kituo hicho kimesajiliwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya dini na usajili wake unaonyesha kuwa kina watu zaidi ya Mia Tatu.

Mwezi Septemba mwaka huu, kituo kingine kama hicho kiligunduliwa katika mji wa Kaduna, kituo ambacho pia kilibainika kuwatesa watu waliokua wakishikiliwa pamoja na kuwadhalilisha.