Kimbunga Lekima chazua hali ya tahadhari China

0
397

Serikali nchini China imetangaza hali ya tahadhari katika jimbo la Zhejiang, lililopo  katika Pwani ya mashiriki ya nchini humo, baada ya Kimbunga Lekima kuonesha uelekeo na uwezekano wa kufika katika maeneo hayo kuanzia hapo kesho.

Tahadhari hiyo imetangazwa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya China,  baada  ya kimbunga hicho kinachovuma kwa kasi ya kilomita 190 kwa saa kuathiri baadhi ya maeneo huko Taiwan.

Kufuatia tahadhari hiyo, serikali ya China imeanza kupeleka vikosi vya uokoaji na huduma za dharura katika maeneo ya jimbo la Zhejiang na Pwani ya Mashariki, ikiwa ni hatua za awali za kujiandaa na athari zinazoweza kusababishwa na Kimbunga hicho cha Lekima.

Maelfu ya watu katika maeneo ya Pwani huko Shanghai, nao wameanza kuyahama makazi yao, baada ya kutangazwa kwa tahadhari ya kimbunga hicho.