Watu 26 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kimbunga Amphan kulikumba eneo la mashariki mwa nchi ya India na baadhi ya maeneo ya pwani ya nchi jirani ya Bangladesh.
Bangladesh ilikuwa nchi ya kwanza kukumbwa na kimbunga hicho jana, kilichokuwa kikisafiri umbali wa kilomita 175 kwa saa na kisha kuelekea nchini India.
Nyumba nyi-ngi katika nchi hizo hivi sasa hazina huduma ya umeme kutokana na athari za kimbunga Amphan, nyumba kadhaa zikiwa zimebomolea, barabara kuharibiwa na miti mikubwa kung’olewa na mingine kuziba barabara.