Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim jong Un amewasili Nchini China kwa ziara ya siku nne .
Akiwasili mjini Beijing kwa kutumia usafiri wa treni Kim amepokelewa na vingozi mbalimbali wa serikali ya china na baadae anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Rais Xi Jinping katika ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo.
Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ameianza ziara hiyo leo huku ikiwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, ambapo anatimiza umri wa miaka 35.
Ziara hiyo inafanyika huku maandalizi ya mkutano wa kilele kati ya kim na rais Donald Trump wa marekani yakiendelea.
Habari zinaeleza kuwa maafisa wa Marekani na Korea Kaskazini wamekutana Vietnam kujadiliana kuhusu eneo utakapofanyika mkutano huo kati ya viongozi hao wawili.